Sponsor

banner image

recent posts

UNGEFANYA NINI?


Mwanamke alimkimbia mumewe na akamuachia mtoto
mwenye miaka mitatu.
Sababu kubwa ya kumkimbia mumewe ni kwamba alipata
boyfriend mwenye hela ambaye alikuwa akiishi Michigan
huko Marekani.
Huyo Boyfriend au mchepuko wake walijuana kupitia
mitandao ya kijamii. Walizoeana sana na mwisho yule
boyfriend wake akamuahidi kumtafutia viza ya kuishi
Marekani.
Na kweli baada ya miezi kadhaa yule mwanamke alimtoroka
mumewe na kutokomea Marekani, huku akiacha taarifa
kwamba asitafutwe tena, anaenda kuanza maisha mengine
mapya. (mumewe alifirisiwa kutokana na kutuhumiwa
ubadhirifu wa mali za kampuni alikokuwa akifanya kazi).
Kutokana na msongo wa mawazo na upweke kwa kipindi
kirefu tokea mkewe amtoroke, yule mwanaume akaamua
kuoa mke mwingine.
Kwa bahati mbaya yule mwanamke mwingine aliyeolewa
hakuweza kushika mimba. Hata hivyo yule mwanamke
mwingine alimtunza vema mtoto wake wa kambo kama
mwanae vile.
Miaka michache baadae, yule mume alifariki kwa ajali ya gari
alilokuwa akisafiri nalo kwenda kijijini kufanya biashara ya
mazao.
Mke wake wa pili alifanya kila jitihada kwa uwezo wale wote
kumsomesha yule mtoto, na Mungu hakunyimi vyote kwani
yule mtoto alikuwa na uwezo mkubwa wa kiakili.
Mwanamke aliuza nyanya sokoni, alitembeza ndizi, alichoma
mahindi barabarani na kadharika ilimradi aweze kujitunza
yeye na yule mtoto wake wa kufikia.
Yule mtoto alijua kwamba yule ndiye mama yake halisi na
ndiye aliyekuwa akimuita mama.
Mama yake halisi aliyetorokea Michigani, Marekani, hakuwahi
hata siku moja kutuma salamu au kuwasiliana na mtoto
wake, ingawa alipata habari kwamba mumewe wa zamani
alifariki kwa ajali.
Miaka mingi ilisonga na kijana alikuwa kwa akili na kimo,
alikuwa Chuo kikuu akisomea Uhandisi wa mafuta na gesi
(Bachelor of science in petroleum Engineering).
Mama yake halisi aliyeko Marekani hakuweza kupata mtoto
tena na yule mwanaume mwingine aliyemuoa, na kwa hilo
yule mume wake mpya aliamua kumtimulia mbali.
Kwa kutambua kuwa alifanya kosa kumkimbia mwanae,
aliamua kurudi nyumbani kumtafuta mwanae na kumkabidhi
utajiri alioupata akiwa Marekani (gawiwo la nusu kwa nusu la
mali baada ya kutalikiana na mumewe wa Marekani)
Bahati mbaya alifika na kumkuta mwane akipigania kati ya
uhai na kifo kutokana na kufeli kwa figo zake. Madaktari
walikuwa wakihitaji pesa nyingi kwa ajili ya upasuaji, pesa
ambazo mama yake wa kambo alishindwa kabisa kuzipata.
Mama yake halisi kutoka Marekani aliingilia hilo suala na
kulipa pesa zote za hospitali kwa ajili ya matibabu, pia
akatoa figo yake moja na maisha ya kijana yakawa
yameokolewa.
Baada ya matokeo ya mwisho ya chuo kikuu kutoka, kijana
alipata ufaulu wa hali ya juu (first class degree) na akapewa
ufadhili wa kwenda kusomea shahada ya uzamili (master's
degree) na baada ya hapo udaktari wa falsafa (phd) huko
Burnley, Uingereza.
Katika kupokea cheti chake siku ya mahafali chuoni kwao,
makamu mkuu wa chuo alimpa kipaza sauti kijana na
kumwambia amuite mama yake katika stage na kupokea
cheti cha heshima.
Baada ya makamu mkuu wa chuo kusema hayo, mama yake
halisi aliyemkimbia alisimama na kujiweka sawa kusubiri
kuitwa na mwanae, wakati mama yake wa kambo aliyemlea
tokea mdogo akiwa bado amekaa huku machozi mengi
yakimtoka huku akimuangalia mwanae wa kufikia kule mbele.
Jibu naliacha hewani.........................
Fikiria wewe ndio huyo mtoto, utamuita nani aje kule stejini
kupokea hicho cheti?
A) Mama wa kambo
B) Mama mzazi
Nahitaji majibu yenu, kama huna share kwa wengine waje na
majibu.
Share
UNGEFANYA NINI? UNGEFANYA NINI? Reviewed by Love Psychologist on March 18, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.