Sponsor

banner image

recent posts

Anataka Kufa Huyu : Nina uhusiano na mke wa mtu. Natamani kumuacha lakini inakuwa ngumu



Wanajamvi umofia kwenu,kwa wakristu wenzangu heri ya Pasaka
Naomba nisiwachoshe. Binafsi nimeoa,nna mke naishi na familia yangu vizuri tu. Lkn nina hili tatizo ambalo kwa sasa limekuwa kero kubwa sana kwangu.

Mm ni kijana wa zamani kidogo umri wangu ni 40+ lkn huyu binti umri wake ni 25. Nilianza kudate naye tangu mwaka 2016. Huyu binti aliolewa mapema sana aliolewa mwaka 2011,baada tu ya kumaliza elimu ya Msingi. Na mwaka 2013 akawa amepata mtoto. Amedumu ktk hiyo ndoa hadi mwaka 2015 akaachika baada ya kushindana tabia na mwanaume huyo.

Baada ya kurudi kwao,ndio nikabahatika kukutana naye kuna siku alikuja ofisini kwangu kupata huduma,akanivutia na tukaongea mawili matatu kisha tukapeana contact safari ikaanzia hapo. Na tarehe 14 February mwaka 2016 rasmi nikaanza kudate naye.

Aisee kwanza sikutegemea kama ningeweza kudumu naye kwa kipindi kirefu kwa jinsi nilivyokuwa namchukulia.

Lkn ndo hivyo nimejikuta nipo naye hadi leo. Sikuwahi kumuahidi kumuoa. Mwaka juzi 2017 mwishoni,akachumbiwa,me hakuniambia. Alichumbiwa mwezi wa 11. Baada ya kuchumbiwa,kwa kiasi fulani akapunguza usumbufu kwangu na mimi wala sikumfuatilia. Lkn siku moja mwaka jana,akaja ofisini akinilalamikia me namchunia na maneno meengiii...!!

Siku hiyo alibaki hapo hadi muda wa kufunga. Nikafunga nikaenda naye kupiga show,me nikamuacha lodge nikaenda kulala kwangu,lkn siku hiyo ndio akaniambia km anataka kuolewa. Aisee,nilifurahi sana moyoni. Lkn akaniambia anataka idhini yangu,kama nipo tayari aolewe lkn nisimuache.

Kwa vile me nilijua anaenda kuwa mke wa mtu, nikamwambia asijali. Huku me nikijua kabisa hii ndo nafuu yangu. Kweli taratibu za ndoa zikaendelea na hatimae akaolewa mwaka jana mwezi wa 8.

Cha ajabu nilivyoona kweli anaolewa,kuna hali ya wivu ikaanza kuniingia. Siku ya ndoa ilikuwa Jumamosi,nikamlazimisha siku moja kabla ya ndoa lazima nipige mashine,demu akasema wewe tu yaani hata ukitaka siku yenyewe. Nikamwambia basi tufanye siku ya ndoa mapema alfajiri.

Me nikaenda kulala lodge ya karibu kabisa na huko kwao,nikampa maelekezo kweli saa 11 alfajiri akapiga simu anakuja. Nikapiga mashine hadi saa 2 asbh.

Binti akaolewa kweli. Tangu siku hiyo ya Jumamosi hakupatikana kwenye simu. Tulikubaliana kwamba,akiolewa atakaa ndani siku 7.( Nasikia hizo siku huwa ni za fimbo tu). Lkn demu kwa mazoea ambayo alishajijengea kwangu,alishindwa kumudu zile kumaliza zile siku 7. Jumatano tu ya wiki iliyofuata akanitafuta na tukaonana.

Tukayajenga na kesho yake mzigo nikapiga tena.

Tumefanya mengi sana na huyu dada lkn sasa kusema kweli,najisikia vibaya sana naona namnyanyasa sana huyu dogo aliyemuoa.

Maana mwanamke kwa sasa kawa kama mtumwa kwangu. Yaani hata akiwa na mumewe ukimwambia njoo,hata kama alikuwa anapika ataacha kila kitu.

Kiukweli nimeshajaribu sana kumwambia tuachane lkn inashindikana kwa sababu ya jinsi tulivyozoeana. Uhusiano wetu hata mama yake anaujua.

Natamani sana nimuache lkn nashindwa. Nitumie njia gani ambayo haitakuwa na madhara kwa pande zote!?? Yaani huwa namhurumia sana jamaa,mfano demu nikiwa naye jamaa anapiga simu hazipokelewi.

Mfano juzi hakuenda kazini,mchana akaja tukawa wote,baadae mumewe akawa anapiga simu lkn simu ikawa silent,na wakati huo sisi tunafanya yetu. Alivyopiga simu sana na simu haipokelewi,akatuma SMS akisema mwambie achomoe kwanza upokee simu..! Nilijisikia vibaya sana,na baadae demu alivyofika nyumbani akaongea naye akasema alitoka lkn simu aliacha ndani,maana jamaa alikuwa kazini.

Na jamaa hagusi kabisa simu ya mkewe. Na demu huwa hafuti SMS wala picha zetu na anajiamini kwa sababu simu ina password.

Kiukweli me kwa sasa natamani kumuacha maana hata mke wangu alishahisi kama natembea naye.

Naombeni nichukue njia gani kuachana naye!??

Nawasilisha kwenu.
Anataka Kufa Huyu : Nina uhusiano na mke wa mtu. Natamani kumuacha lakini inakuwa ngumu Anataka Kufa Huyu : Nina uhusiano na mke wa mtu. Natamani kumuacha lakini inakuwa ngumu Reviewed by Love Psychologist on April 22, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.