Sponsor

banner image

recent posts

Mi Sijawahi , Wewe je, Umewahi kuwa dilemma?



Ni hivi, nina marafiki wawili wa kiume na wa kike. Wote ni marafiki zangu na nimefahamiana nao kwa vipindi tofauti. Wa kike naomba nimuile Lulu na wa kiume Frank.

Kutokana na kuwa nao karibu niligundua wana vitu vingi wanavyoshabihiana, hivyo kwa namna moja au nyingine nilihusika kwa wao kuwa wapenzi.
After a while niligundua Lulu anamcheat Frank as alikuwa na mahusiano na mwanaume mwingine. Nilipomuuliza aliniambia niuchune na Frank akijua atajua ni mimi nimemwambia. Japo nilijaribu kumsisitiza kuwa ipo siku atajua tu sio lazima mimi kumwambia.

Kweli za mwizi 40, Frank akagundua na ugomvi ulikuwa mkubwa sana. Taabu ikaja Frank ananilaumu kuwa lazima nilijua na sikumwambia hivyo ananiona rafiki nisiefaa. Upande wa Lulu anakazana kuwa mimi ndio nimemwambia Frank na shutuma nyingine nyingi tu.

Sasa kila upande unaniona mbaya wake

Umewahi kukutwa na situation ya hivi? Ulifanya nini?

Mi Sijawahi , Wewe je, Umewahi kuwa dilemma? Mi Sijawahi , Wewe je, Umewahi kuwa dilemma? Reviewed by Love Psychologist on April 22, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.