Sponsor

banner image

recent posts

Chozi la Damu: Mateso apatayo mwenye jini mahaba


Ilikua siku ya kawaida tu katika mtaa wetu mara mbele yangu akatoea mzee wa makamo mwenye umri wa kustaafu alionekana ni mtu aliesawijika huku uso wake ukigubikwa na huzuni na kuanza kunisalimia bila ya mda kupita akaniambia lengo lake kuja kwangu, aliniambia tokea kijana wake aingie katika ndoa yapata miezi 3 hajakutana na mkewe kutokana na matatizo alionayo huyo mwanamke.

Kwangu mimi alikua akihitaji cheti cha dawa ambacho kinaweza kumsaidia akapata dawa aina ya viagra ili aweze akampatie kijana wake aweze kubusti uume wake huku wao wakiendelea na tiba nyengine. Nilimuahidi kumpatia hizo dawa wala asingehitaji hicho cheti.

Kwakweli sikumuuliza nini haswa kitu gani kimempata kijana wake kwa vile kesi hizi masikioni mwangu sio ngeni na nimewashuhudia wengi wakimwagika machozi kwa simulizi zao zenye kuhuzunisha. Hapa sina lengo la kusimulia hadithi bali ni kuweka wazi ni yepi haswa ambayo huwa yanawapata.

Katika hali ya kawaida haiwezekani mtu kumuona jini labda na yeye awe anaye huyo jini, ila kwa alie na jini mahaba basi kwa hatua yake ya mwisho anaona nae huyu jini na kuweza kuishi nae maisha ya kawaida.

WAKATI WA TENDO LA NDOA
Ikiwa mwanamke ndio mwenye huyu jini ,mume wake anapotaka kumuingilia huwa anaona ile sehemu ya siri ya mkewe ipo kama ya mtoto mdogo hivo anawacha halafu jini anafanya mambo yake, wakati mwengine huwa hauoni kabisa na ile sehemu (uke) huwa kama kipande cha ubao.

Si hivyo tu bali muda mwengine mwanamke huwa anatoka na damu nyingi na kumsababishia mume wake kutokua na hamu ya tendo. Vituko vyote hivi jini huvifanya ili aweze kumzuia mume asimkurubie mke ili aweze kustarehe nae yeye tu.

Ikiwa mwenye jini ni mwanamme wakati wa tendo la ndoa jini huusababisha uume wa mwanamme kusinyaa punde tu anapotaka kumuingilia mke wake, ikiwa mwanamme hajaoa basi kuoa itakua vigumu kwani mke wake huyu wa kijini huwa anampatia hata pesa ili mradi tu atulie na yeye.

Ikumbukwe pia jini ananguvu zaidi katika tendo kuliko hata mwanaadam.

Natumai utakuwa umeyapa alau kwa ufupi yanayowafika wenye jini mahaba, kama utakua na swali niulize.
Chozi la Damu: Mateso apatayo mwenye jini mahaba Chozi la Damu: Mateso apatayo mwenye jini mahaba Reviewed by Love Psychologist on April 16, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.