Sponsor

banner image

recent posts

Dalili kuwa mtoto wako anatumika kingono.



WATOTO WANATUMIKA KINGONO!
Inaumiza lakini ndio uhalisia! sio kitu kinapendeza machoni wala akili lakini ndio ukweli!

Watoto wetu hawako salama!

Hawako salama sio kwa watu tunaoamini sio salama.

Watoto hawako salama kwa watu tunaoamini wako salama!



Kuna vitu tu lazima kama jamii tuambiane na tuinue sauti kuvizungumza!

Unyanyasaji kingono miongoni mwa watoto ni jambo ambalo lipo, linafanyika, linatendeka under our very noses!

Ni vile tu hatuamini na tunafikiri wapo salama! ni vile tu tunaamini sio kitu kinaweza kutokea kwa wanetu! ni vile tu tunaamini wapo watoto aina fulani wa kufanyiwa hayo!



Sio kweli!

Sio kweli!

Sio kweli!


Leo hebu tushirikishane dalili ambazo zinaweza kuwa taarifa kuwa mtoto anatumika kingono.



Unyanyasaji kingono umekuwa ni sehemu ya historia za maisha ya baadhi yetu.



Matukio yote unayokumbuka ulifanyiwa ukiwa mdogo ambayo leo ukiwa mtu mzima

unaweza kuyahusisha na matukio ya kingono na hukusema ndiyo hayo yanaweza kuwa yanamtokea mtoto sasa na hasemi.



nyingine ni

Mtoto anapata shida kukaa au kutembea (2 - 10yrs)
Anaogopa kupita kiasi baadhi ya watu, mahali au vitu (0-5yrs)
Anapenda kujishika sehemu za siri kiasi cha kujisahau mpk kulala akiwa anajishika.
Anakaa chooni muda mrefu au kuhitaji kujisaidia mara kwa mara.(0-5yrs)
Anaweweseka usiku (0-5yrs)
Anakataa/kusumbua kula au kutapika bila ugonjwa mahsusi. (0-5yrs)
Analia sana (0-3yrs )
Anaona aibu na kujitenga (umri wote)
Anashindwa kuzuia haja kubwa (4-7yrs)
Anakuwa mkimya isivyo kawaida (umri wa balehe)
Anashuka kielimu (6-17)
Anakuwa na kiburi, maamuzi ya kukinzana na maagizo( umri wa balehe)
Mimba (11-17)
Majaribio ya kujiua (8- 17)
Anakimbia nyumbani mara kwa mara (8-17)
Msongo wa mawazo (8-17)
Anakataa kushiriki shughuli za nyumbani, za shule, za kiroho. (7-17)




Ongeza zingine na tushauriane cha kufanya!

Dalili kuwa mtoto wako anatumika kingono. Dalili kuwa mtoto wako anatumika kingono. Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.