Sponsor

banner image

recent posts

KUCHEPUKA: Hakuna mwanaume rijali atakayevumilia kuwa na mwanamke mmoja tu



Kama utakwazika kwa namna moja ama nyingine naomba uniwie radhi mana hata mimi sipendi sana kuyaongelea haya mambo ila naomba tu dada zetu mtambue kwamba ukweli unaoumiza ni bora kuliko uongo unaofurahisha.

Ukweli ni kwamba hakuna mwanaume wa aina hiyo hasa karne hii hivyo usije ukadanganyika kujiingiza kwenye ndoa ukiamini kwamba utaenda kujimilikisha huyo mwanaume akawa wako peke yako.

Mwanaume ameumbwa kuwa na na wanawake wengi na hiyo ni human nature.Kinachomata ni suala la muda tu mana inawezekana umeishi na mume wako kwa zaidi ya miaka mitano au hata kumi kwenye ndoa na hujamkamata na dalili zozote za kuchepuka lakini tambua kwamba sisi wanaume tuna usiri mkubwa sana pindi tunapoamua kufanya yetu.

Kuchepuka kwetu sisi wanaume haimaanishi kwamba hatuwapendi wake zetu hapana ila tu tuna ile hali ya tamaa ya kutaka kujaribu radha tofauti tofauti na kama mnavyojua kwamba idadi ya wanawake ni kubwa kuliko wanaume.

Sipo hapa kwaajiri ya kuhamasisha wanaume wenzangu wachepuke hapana ila ni kujaribu tu kuwakumbusha dada zetu kwamba haya mambo yakuchepuka kwa wanaume ni kitu cha kawaida mana ukiona mwanaume hachepuki ujue afya yake ina matatizo au hayupo vizuri kifedha kwa wakati huo lakini akizipata ndo utamtambua vizuri kama upendo aliokua anakuonesha ni wakuigiza au ni wakweli.

Kuna mambo mengi ambayo hufanya wanaume wachepuke kama wivu wa wanawake wa kupitiliza , ugomvi wa mara kwa mara, majigambo, matusi na dharau kupita kiasi.Haya ni baadhi ya mambo yanayosababisha wanaume wachepuke na wakati mwingine kwa wale wachache wasio na michepuko hutamani hata kulala maofisini ili tu wasirudi nyumbani.

Ni ngumu sana mwanaume kuwa na mwanamke mmoja sababu mwanamke hawezi kuwa na vyote ambavyo wanaume tunavihitaji.Simaanishi kwamba michepuko iendelee hapana ila huo ndo ukweli wa mambo.Wanawake jitahidini kusoma alama za nyakati ili wenzi wenu wapunguze idadi ya michepuko ila sio kuacha kabisa mana hilo haliwezekani.

Wanaume ambao hawachepuki kabisa ni wale ambao walifariki kwenye vita kuuu ya pili ya dunia.

KUCHEPUKA: Hakuna mwanaume rijali atakayevumilia kuwa na mwanamke mmoja tu KUCHEPUKA: Hakuna mwanaume rijali atakayevumilia kuwa na mwanamke mmoja tu Reviewed by Love Psychologist on April 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.