Sponsor

banner image

recent posts

Ngono/mapenzi kabla ya Ndoa: Faida na Madhara yake...



Mara kwa mara nikuwa nikisikia kuwa ngono hizi zinazofanywa kabla ya ndoa ndio zinachangia kufanya ndoa nyingi zisidumu.

Nimewahi kusikia hivyo kwenye semina za vijana miaka ya nyuma kidogo ambapo vijana walihimizwa kuhakikisha wanatunza miili yao hadi pale watakapounganishwa na ndoa na kuwa mme na mke halali.

Jana tena nikiwa nasoma kitabu fulani cha kiingereza kinachozungumzia masuala ya maisha ya ndoa, nimeona msisitizo kama huo nikajisemea kuwa hapa kuna namna ambayo huenda vijana wa sasa hawaelewi.

Ni kwamba inasemwa kuwa tendo la ndoa linalofanywa na wahusika siku ya kwanza linakuwa na msisimko wa aina yake kuliko tendo lolote litakalofuata, ndio maana inasemwa kuwa si rahisi mwanamke kumsahau mwanaume aliyefanya naye mapenzi siku ya kwanza.

Kama hivyo ndivyo wewe kama mwanaume au mwanamke unategemea mwenzako akuone wa pekee kuliko yule aliyekutana naye kimwili mara ya kwanza? Kama sivyo basi kila mmoja anawajibika kwa usaliti wake kwa mwenzake ambaye pengine kwa sasa bado hujamfamu, je unapolilia kusalitiwa umejiuliza uliwahi kusaliti mara ngapi?

Kama tunaamini kuwa kila mtu aliwekewa mtu wake tangu alipozaliwa basi kwa vyovyote vile ufanyavyo kabla ya kuoa/kuolewa unakuwa ni msaliti kwa huyo mtu ambaye pengine kwa sasa bado hujamfahamu, au ikiwa umeoa/kuolewa lakini uliwahi kujihusisha na ngono na me/ke mwingine na wewe pia ni msaliti hivyo huna haki ya kulalamika pale msaliti mwenzako anapokufanyia usaliti.
Ngono/mapenzi kabla ya Ndoa: Faida na Madhara yake... Ngono/mapenzi kabla ya Ndoa: Faida na Madhara yake... Reviewed by Love Psychologist on April 25, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.