Sponsor

banner image

recent posts

Maisha ninayoishi ni ya ajabu kweli, ushauri wako unahitajika




Wakuu, hili jambo utakalolisoma hapa ni maisha yangu 100%.

Kuna ile kauli mtoto umleavyo ndivyo akuavyo, naona ni kweli 100%. Haya maisha ninayoishi sehemu kubwa ni matokea ya makuzi yangu.

Nimekulia kwa kiasi kikubwa ila sio saana kwa mjomba wangu ambae ni mchungaji mmoja mkubwa wa madhehebu ya Assemblies of God.

Pamoja na kwamba mimi siamini mungu tena ila maisha ya pale kwa mjomba yameshape kwa kiwango kikubwa maisha ninayoishi sasa, ambayo kwa ujumla siyapendi ila nimeshayazoea na nimeshindwa kuyaacha.

Sipendi kutoka nyumbani, sipendi kusocialize(kwa kiasi flani sasa najitahidi), naweza kushinda nyumbani peke yangu ndani hata siku 5 kama nina hiyo nafasi, naweza kuishi na majirani wasijue niko ndani siku 3, labda wanione natoka kwenda mtaani kununua hitaji flani ila kama kila kitu kipo ndani sitoki.

Napenda kulala, naweza kutoka kazini labda sa 10 kama nimewahi kutoka, nimifika nyumbani nafunga milango naingia room kulala hadi kesho yake au labda nihisi njaa na ndani chakula kiwe kimeisha ndio naweza kutoka. Sipendi kabisa kutoka, nikiwa na msichana ntamshindisha ndani hata wiki, wengi wanashindwa aina ya maisha yangu.

Nyumbani kwangu nina kila kitu maana nina kazi inayoniwezesha kuishi ninavyotaka, lakini cha ajabu hata sebuleni sikai, sebuleni kwangu kuna kila kitu kizuri lakini naweza kumaliza mwezi sijakaa sebuleni labda aje mgeni kunitembelea.

Hata ndugu wakinitembelea, wakikaa siku zaidi ya moja tunaweza kujumuika siku ya kwanza au ya pili tu, baada ya hapo naweza kushinda nimelala wao wako sebuleni na vyumbani kwao. Ndugu wengi wameshanizoea hvyo maana wamejaribu kushauri ila sibadiliki.

Haya maisha ya kutopenda kutoka nime adopt kwa mchungaji, alikua hataki tutoke kwenda senta, hvyo kama umemaliza shughuli zako ujisomee ukichoka kalale, tokea hapo nimekua hivyo. Ilikua ni marufuku kutoka kwenda mahala popote bila sababu ya msingi labda utumwe.

Nakumbuka hata baada ya kumaliza elimu ya chuo kikuu miaka kadhaa iliyopita nilikua nashinda nimelala tu, brother akaniambia nijichanganye na watu nisiwe peke yangu, hapo ndio mara yangu ya kwanza nikaanza kwenda bar na kukaa muda mrefu na kupitia hapo ndio nikakutana na mkurugenzi wa utumishi ninapofanya kazi akaniajiri, isingekua ushauri wa bro labda ningekua mtaani hadi sasa, labda..

Haya maisha ninayoishi siyapendi ila sijui kama nitabadilika maana nimekua mtu mzima sasa, miaka 30.

Hivi kuna mtu ana namna ya kuniahauri nawezaje kubadilika?
Maisha ninayoishi ni ya ajabu kweli, ushauri wako unahitajika Maisha ninayoishi ni ya ajabu kweli, ushauri wako unahitajika Reviewed by Love Psychologist on April 01, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.