Sponsor

banner image

recent posts

Mengine mnajitakia wakina dada



Hebu twende kwenye mada tu.

Jamani

Juzi tu nimetongoza mwanamke flani hivi. Namshkuru Mungu pamoja na kasumba zangu lakini akakubali.

Hee
Baada ya siku mbili akanambia kiwa anadaiwa Kodi ya nyumba elfu 90. Nikamwambia powa ntakupa.

Mh
Siku ilofuata akasema ana shida Sana ya sabufa hivyo nimnunulie. Nikamwambia sawa usijali.

Wakati huo huo
Akadai Hana pesa ya Kula... Hapa ikabidi nimkatie fungu nono ili akidhi mahitaji yake ya chakula japo kwa wiki mbili mbele.

Baada ya siku moja
Akadai kuwa simu yake ni mbovu hivo nimpe pesa ya kuipeleka kwa fundi au nimnunulie nyingine.

Kumbuka hapo Bado sijapewa papuchi, na nikiomba nasogezwa mbele siku kama bicon ya upanuzi wa barabara.

Leo akaanza kutaka kujua nalipwa shilingi ngapi kibaruani kwangu.... Duh nikaona hapa hakuna changu.

Nilichofanya Ni kumpa uwazi tu kuwa WEWE HUNIFAI KWAKWELI

KILICHOFUATA
Akaanza kulalamika kuwa ana mikosi na wanaume, kila mwanaume anamuacha.

Sasa nikajiuliza
Kwa tabia hii ni mwanaume gani atakuvumilia? Huna hata staha Basi?

Hivyo Basi
Mambo/mikosi mingine mnajitakia wenyewe akina dada.

Uzi tayari

Mengine mnajitakia wakina dada Mengine mnajitakia wakina dada Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.