Sponsor

banner image

recent posts

Unapokosea step kwenye kumpata mwana ndoa



Tukiwa wadogo mmoja wa majirani zetu alikuwa mtu mzito serikalini, enzi zile nilisikia alisomea shahada yake ya uchumi Makerere Uganda.

Alikuwa na mke mrembo sana, nilisikia pia wakati akiwa chuoni huko Uganda, akirudi likizo na kumpa ujauzito binti mmoja kijijini kwao. Wazazi wa yule binti walimsusa mtoto wao kwa wazazi wa bwana yule. Hivyo alivyohitumu masomo alikabidhiwa mke.

Sasa wakati ule wa ujenzi wa makao makuu Dodoma yule Baba ndiyo wana uchumi waliokuwa wanaaminiwa na kupelekwa Dodoma. Familia ilibaki Dar. Kwakweli yule mama staha hakuwa nazo. Alikuwa mlevi mbwa, tofauti na heshima ya yule mzee aliyokuwa nayo.

Kule Dodoma mzee alitengeneza pesa sana. Lakini kwa kanuni za uongozi alishindwa kuanzisha miradi. Alianzisha biashara kubwa kwa jina la mkewe. Yule mama alishika pesa nyingi sana. Baba alipostaafu mkewe alimwambia huna chako hapa kila kitu ni mali yangu.

Yule mama alipata kijana kutoka nchi jirani alimuoa na kuondoka na mali yote. Alirudi akiwa mahututi baada ya kuambukizwa HIV na wakati huo ilishafikia kwenye AIDS.

Yule baba alimuuguza kwakua alikuwa mstaarabu. Mwisho wa yote alifariki.

Unapokosea kutafuta mwenza ni majanga.
Unapokosea step kwenye kumpata mwana ndoa Unapokosea step kwenye kumpata mwana ndoa Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.