Sponsor

banner image

recent posts

SIRI KUBWA: Hitaji kubwa la mwanaume ndoani ni kuheshimiwa hata pale anapokuwa amekosea



Wanawake wenzangu, kila siku napenda kuwaweka wazi mambo muhimu sana katika mahusiano na ndoa zetu.

Leo nataka nikukumbushe tena jambo hili. Kama unaona ndoa au mapenzi yako yanayumba yumba lakini mwanzoni yalikuwa na furaha na uliyafurahia, basi inawezekana kabisa kuna mahali uliyumba ama ulianguka hasa katika kipengele cha kumheshimu mumeo.

Nisikilize my dia, hitaji kubwa la mwanaume katika ndoa yake ni kuheshimiwa zaidi na mkewe. Tunapozungumzia heshima kwa mwanaume, katika mazingira yetu, tunamaanisha hali ya kutamani kujiona yu na hadhi ya juu, yu na mamlaka zaidi pengine kuliko mwanamke.

Kinyume chake ni kudharauliwa, kuwekwa katika mazingira ya kujiona hana hadhi, hana mamlaka, asiye na kauli wala uwezo kufanya lolote bila mwongozo wa mwanamke.

Kwa wanaume wengi, heshima ni namna unavyoongea nae, maneno unayoyatumia katika kueleza mawazo yako, ishara za mwili wako katika mazungumzo, kumpa nafasi ya kwanza katika maamuzi na mambo kama hayo.

Heshima, vile vile, ni kumstahi mwanaume unayempenda hata anapokosea. Kosa linapotumika kama sababu ya kufanya vitendo vinavyodhalilisha hadhi yake ni kujipunguzia alama. Ndio kusema, staha ni kuong
ea naye kwa nidhamu hata katika mazingira ambayo ni dhahiri yeye ndiye mkosaji.

Kadhalika, heshima ni kuwa tayari kumtunzia hadhi yake kwa watu wengine. Kumjengea taswira inayomwongezea thamani yake kwa watu unaojua anawaheshimu. Kuonesha fahari yako kwake unapoongea na watu wengine kwa kauli, matendo na hisia kunaongeza alama za sifa anazozihitaji kwa mwenza wake.

MWANAMKE LIELEWE HILI NA UJITATHMINI
SIRI KUBWA: Hitaji kubwa la mwanaume ndoani ni kuheshimiwa hata pale anapokuwa amekosea SIRI KUBWA: Hitaji kubwa la mwanaume ndoani ni kuheshimiwa hata pale anapokuwa amekosea Reviewed by Love Psychologist on April 22, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.