Sponsor

banner image

recent posts

Swali kwa wanaume



Habarini!! I hope mko poa.
Nina swali haswa kwa wanaume, ila kina mama/dada pia mnaweza changia.
Humu kuna threads kibao waliojifunza mapenzi/kujamiiana kwa wadada wa kazi nyumbani, wengine mlianza mkiwa wadogo sana. Mila yetu kiAfrika tunaona kama huo ndio uanaume ila damage ni kubwa sana. Kuna comment zingine mtu anaandika umri aliozini kwa mara ya kwanza na dada, kiukweli, baadhi yenu mlikuwa abused, maana si kitu cha kufagilia kwasababu kwa umri uliokuwa nao, dada ndio alikuwa mtu mzima na wewe ndio ulikuwa mtoto. Usikute somewhere out there, yule dada aliondoka na uja uzito wako bila wewe kujua umefanya nini.

Swali langu ni, je ukijua leo hii, dada wa kazi anazini na mtoto wako wa kiume, utachukua hatua gani? vuta fikra mtoto wako wa kiume yuko chini ya umri wa miaka 10 na mwingine miaka 10-17.
Unamuelimishaje mtoto wa kiume? Hii karne imeharibika sana, malezi yetu na watoto wa leo ni vitu viwili tofauti.
Swali kwa wanaume Swali kwa wanaume Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.