Sponsor

banner image

recent posts

Umewahi kufikiri kuhusu usalama wa watoto wako kijinsia?



Tafiti na shuhuda nyingi zinathibitisha usalama finyu wa kijinsia unaowakabili watoto.

Leo tutizame maeneo HATARI ZAIDI KWA WATOTO
Haya ni MAENEO YANAYOFIKIRIWA KUWA NI SALAMA KABISA!
-MAJUMBANI.
Watoto huharibiwa zaidi na ndugu, kaka zao, dada zao, mabinamu, babu, baba, mama, wajomba, baba wadogo, mama wadogo jamaa marafiki wazazi, majirani, watoa huduma kama nannies.

(TUKIPITISHA KURA HAPA WENGI WETU BIKRA ZA KIUME NA KIKE ZIMETOKA CHINI YA PAA LA NYUMBA YA BABA ZETU, wanaume ni mashahidi zaidi wa hili, namna walivyojifunzia ngono mapajani mwa dada zao waliokuwa wanawalea, UNAFKR MWANAO HALIWEZI KUMKUTA?UMEWAHI KUFIKIRI NAMNA YA KUMLINDA , AU NAMNA YA KUMSAIDIA AKIPATA THE SAME SAGA ULILIPATA? ANAWEZA KUKWAMBIA?)

-MASHULENI
Walimu, wanafunzi wenzao, wahudumu wa shule kama madereva wa magari, matrons/patrons, viongozi wa madarasa,viongozi wa mabweni. Watoto huamini walimu wao sana, watoto huamini wezao sana, watoto hutumia muda mwingi shuleni kuliko nyumbani! Kile mzazi atasema ,ili kiwe na mashiko ni lazima mwalimu au anko wa shule akisisitize! UMEWAHI KUFIKIRI KUHUSU HATARI YA MWALIMU NA ANKO WA SHULE ANAMWAMBIA NINI MWANAO? UMEWAHI KUWAZA IWAPO HABARI UNAZOSIKIA ZINATOKEA KWA WENGINE PENGINE NA MTOTO WAKO ANAAMBIWA MANENO YALE YALE? UNAJUA NAONGEA NINI NA WENZIE? ANA TAARIFA KINZANI YENYE UKWELI KUHUSU LOLOTE ANALOAMBIWA KIASI LISISHIKE AKILI YAKE?



-NYUMBA ZA IBADA
Walimu wa dini, makasisi, mashekhe, wahudumu wa kanisa na misikiti. Elimu duni pembeni hii ni elimu ya kiroho! Kama vile umwaminivyo kiongozi wako wa kiroho , ndivyo na yeye mwanao anavyomztizama pengine kama mungu(kulingana na anachoelewa kuhusu mungu)USIWAZE POPOTE KUWA KUNA KITU ATAAMBIWA NA KIONGOZI WA KIROHO AKATAE! kwanza kwa imani pili kwa vitisho! Tena akipitia mistari na nukuu zile zile.
-MTAANI
Vyombo vya usafiri, mitandao ya kijamii, vichochoro vya njia, makondakta , madereva, bodaboda, bajaji, wauza maduka, wauza vitu vya kula kama chipsi, lambalamba, ubuyu, kashata , ice cream, chama.


HAYA NI MAENEO TU.
Kuna IMANI ZA KISHIRIKINA , kuna MIHEMKO YA UMRI, kuna ELIMU RIKA POTOFU, kuna MIKUMBO NA KUIGA.

KWA KIFUPI HAWAPO SALAMA!
HAWAPO SALAMA!
HAWAPO SALAMA!
Weka nukta, puuza, ona ni ya kupita , ona halikuhusu LAKINI MY DEAR WATOTO WETU HAWAPO SALAMA!

TUFANYE NINI?
TUPEANE MAWAZO!
Umewahi kufikiri kuhusu usalama wa watoto wako kijinsia? Umewahi kufikiri kuhusu usalama wa watoto wako kijinsia? Reviewed by Love Psychologist on April 08, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.