Binafsi nilijaribu kuchepuka ( dhambi kwa mujibu wa imani yangu, na nimetubia hii dhambi sitoirudia tena hadi nakufa).
Huwa anajua nikibanwa na majukumu sana na muda ukiwa umeenda huwa nachukua hotel napumzika na huwa nampa taarifa, ni mwanamke na mama aliyetokea kuniamini sana kama mimi ninavyomuamini.
Sasa usiku mmoja sikuridi na nikawa nimepiga mechi ya nje ( demu wa kuota huko duniani ), wakati narudi home asubuhi, nikamuona mchumba anapita njia ya juu sijui alikuwa anaenda madukani, ikabidi mie nipite njia ya chini kumkwepa, nikakosa kabisa confidence ya kukutana nae wala hata kumsalimia uso kwa uso ( sijui aliona au hakuniona )...
Nikafika home nikaoga, nikawasha laptop nikaanza kupitia mambo mawili matatu, akarudi wala hakuniuliza kitu, akaniandalia chai akaniwekea mezani nae akaja kukaa pale tukaanza kupiga story mbali mbali huku tunakula ( moyoni mwangu nikawa nasema huyu kama akijua nilichofanya usiku wa leo sijui itakuwaje hapa, na cha ajabu mapenzi yake kwangu ndio yakazidi kweli kweli, utani mwingi, cheko nyingi na furaha iliyotamalaki moyoni mwake, ndio nikawa nakosa kabisa amani nikawa nafumba fumba macho kama usingizi vile umenipitia ili nimkimbie nikalale, kabla ya kunipa ruhusu ya kwenda kulala, anapotaka kutoka huwa lazima tupige magoti kidogo tuombe kwa pamoja ndio aendelee na issue zingine.. na kwenye kuomba ukawa mtihani mkubwa zaidi...
Kwa wengine mlipokutana na mazingira haya mlikuwa katika hali gani na mliweza kumudu vipi?
Unapotoka kusaliti (kuchepuka), unapokutana na mwenza wako hivi unajisikiaje?
Reviewed by Love Psychologist
on
April 25, 2019
Rating:
No comments: