Sponsor

banner image

recent posts

Huyu mke wangu aisee! Hivi wanawake wa kihaya ndo walivyo?



Wakuu Toka nimemsafirisha mtoto mzuri kutoka bukoba to mtwara Nina miezi miwili! Nililazimika kuchukua likizo ya mwezi mmoja na nusu ili niwe nyumbani tu na huyu binti!

Sasa muda umefika nataka nichakarike na kazi lakini huyu mke wangu simuelewi! Kila nikitaka kutoka asubui inakua mgogoro Mara ashike kiatu, lengo nichelewe niwe nae tu.

Kazi sifanyiii mbali niko mtaa huu huu lakini najitahidi nirudi mchana kula kimbembe wakati wa kutoka! Nachelewa Mara afiche funguo! Sasa wiki ilopita hapa kazini napoteza wateja na hii wiki ya pili Toka nifungue hi barber shop!

Naomba ushauri kwa wazoef hivi hawa wahaya ndo walivyo yani kila wakati anapenda tuwe sote tu wakati mwingine anakuja hadi kazini! Tunakaa anaenda nyumbani anadai anachoka kukaa mwenyewe wakati Kuna wanawake karibia 5 kule tunakoishi kwa nini asishinde nao?

Huyu mke wangu aisee! Hivi wanawake wa kihaya ndo walivyo? Huyu mke wangu aisee! Hivi wanawake wa kihaya ndo walivyo? Reviewed by Love Psychologist on May 04, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.