Sponsor

banner image

recent posts

True Story: Na hii ndio sababu kwanini situlii na demu mmoja


Leo nimekuja kushare nanyi hii story ofcourse ni muda iko moyoni mwangu ila nimeamua kushare nanyi ili mjue kwa nini kila siku mimi mtu wa kubadilisha wasichana,

Ni hivi miaka Saba Nyuma wakati niko collage jijini dodoma nilikuwa na mahusiano na binti flani hivi alikuwa ni mzuri Aswaa ninaposema mzuri mjue namaanisha, alikuwa mweupe, mrefu flani hipsi na mteke mteke,

Alikuja pale collage kusoma kozi moja na mimi kweli ile siku ya kwanza tu kureport yeye alichelewa kidogo mi nilimuona na kumchangamkia mwisho wa siku tukabadilishana mawasiliano, jioni yake tukayajenga tukawa wapenzi,

Yule binti kwa kweli hakuwa amewahi kufanya mapenzi alikuwa ni bikra na mimi ndio nilikuwa mpenzi wake wa kwanza kushiriki nae tendo,
Mwanzo nilipanga tu niishi nae then nikimaliza niachane nae lakini sijui kwa nini nilitokea kumpenda sana yule binti,

Ninapozungumzia kupenda, ni kupenda kweli wakuu,ila kitu sikuwa najua ni kwamba sidhani kama yeye alikuwa ananipenda kweli au kupretend,
Semister ya kwanza ilivyoisha ndio nikaanza kuona mapicha picha unapiga simu hapokei, tuma text hajibu mambo yake ni kuforce force akitaka kitu, mwisho wa siku aliniambia tu yeye mwenyewe tena kwa meseji kavu kwamba Zero mi sikupendi tena,

Niliumia sana kiukweli kuuliza sababu nini hana ni vile ameamua,
Mawazo niliyokuwa nayo ni zaidi ya milioni sikuwa nakula ata nikila ni chakula kidogo tu, yaani sometime nilitamani ata kujiua ila nashukuru marafiki zangu walikuwa pamoja nami,

Siku zikapita tukamaliza chuo akarudi huko kwao bhana sijui kakutana na nani akapewa Mimba ikiwa na miezi 4 akanitafuta sijui namba yangu alipewa na nani, baba yake amemfukuza sijui hamtaki hana pa kwenda da aisee niliumia sana nilichofanya tu kwa kuwa nilikuwa nampenda kweli,nikampigia mzee nyumbani nikajipa msala nikamwambia mi nimemsababishia mimba mtoto wa watu na amefukuzwa kwao hana pa kwenda wazee wakasema tu nimpeleke kule watakaa nae,

Nilichofanya nikamtumia nauli akaja mpaka nilipo wakati huo nakaa kwa bro na nafanya kazi ya ufrelencer kusajiri laini za tigo, Airtel na Voda, yeye nikamchukua nikampeleka gest na kukaa siku 3,baada ya majadiliano tukaafikiana aende kwa dada yake aliyeolewa mkoa wa jirani na hiyo ni baada ya kuwasiliana nae nikampa nauli akaenda kufika kule kumbe ata sehemu ya kulala hamna wale walikuwa wamepanga ilibidi atafute chumba nikamtumia hela ya kodi,pamoja na ya kitanda na godoro,

Nilihudumia ile mimba mpaka ikafikia miezi 9 kasoro, kila kitu kuanzia kula mpaka vaa yake nilikuwa nagharamia, nilimnunulia Vifaa itajika vya kujifungulia vyote sijui mabeseni, mavitenge na vingine ata kabla ya siku ya kujifungua, ilivyofika miezi tisa mama yake ndio akamtafuta na kusema akajungulie kwao nikatuma nauli akaenda kwao,

Hakubahatika kujifungua kawaida ila kwa oparation na gharama zote nilitoa aisee haya mapenzi haya, yaani kamission yangu yote niliyokuwa napata kwenye kazi ilikuwa inaishia kwake,

Mtoto yule akakua japo homa za mara kwa marahadi alipofikisha miaka 3 kasoro yote nilikuwa nalea kama mwanangu, mwisho wa siku baba yake huyo mpenzi wangu akasema anamrudisha chuo akaendelee na level nyingine na chuo ni mkoa nilipo mimi,

Siku ikafika akatimba kama kawaida tukaendeleza penzi letu, baada ya miezi kadhaa kupita nikaanza kuona tena mabadiliko safari hii ni kwamba hakutafuti mpaka umtafute, sms anajibu short mnaweza kupanga apointment na asitokee bila sababu, ukimpiga simu akipokea unakuta anaongea huku yuko busy na marafiki zake Zero Nikajiongeza tu nikasema hapa deal litakuwa limeisha,

Nami nikakaa cool wiki hakunitafuta siku ananitafuta eti Mambo Nitumie hela ya kula, hakuna cha umeshindaje, aulize ata vipi mbona upo kimya hamna nilimjibu tu sina hela,

Maneno yaliyokuja hapo ni noma kila nikijitahidi nimuelekeze kwa busara wapi mwenzangu haelewi basi nikaona kama naforce mahusiano kwa mtu asiyenipenda mwisho akanitumia Sms kubwa eti sijui yuko busy hataki usumbufu, kama ni gharama zangu nilizotumia kwake atanilipa akimaliza chuo na kupata kazi sijui kama hako ka elfu kumi ninakomtumiaga ka kula baba yake ata handle kwani ana uwezo kama anaweza kumlipia ada ya mamilioni hiyo si kama chai tu, Kwa dharau(hayo maneno huwa nayakumbuka mpaka leo )

Ofcourse mimi kwetu hatukuwa na Uwezo,na ata chuo nilishindwa kuendelea na level nyingine kwa sababu mzee hakuwa na uwezo ila kitu alichokosa kukijua ni kwamba kila senti niliyokuwa nampa ni kati ya Asilimia 90 ya kipato changu kwa wakati ule nilijibana ili nimuhudumie yeye, kuna muda nilishindwa kujiwekea Akiba au ata kusaidia ndugu zangu kwa kumpa yeye kipaombele ila kwa maneno yake nilicheka huku moyoni nikipata maumivu makali kinyamaa,

Kiukweli tuliachana na Sikuchukua muda maumivu yale yakapona niliapa Mimi Zero IQ kamwe sitokuja tena kumpenda mwanamke wa aina yeyote thats why mnaona hivi,

Mabandiko yangu humu jukwaani kwa zaidi ya Asilimia 95% yana ukweli ndani yake,
Na Zero IQ mimi siamini mwanamke wa Aina yeyote nilishasema ata kuoa sijui kama nitakuja kuoa mimi ni kupiga na kusepa tu ata uwe mzuri vipi maybe hapo mbele naweza kuchange baada ya kufikia umri fulani ila sidhani.



Hiyo ndio story yenyewe wakuu.

True Story: Na hii ndio sababu kwanini situlii na demu mmoja True Story: Na hii ndio sababu kwanini situlii na demu mmoja Reviewed by Love Psychologist on May 10, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.