Sponsor

banner image

recent posts

Huu ndio mtazamo wangu katika mahusiano ya mapenzi siku hizi.

Katika Maisha kila mtu ana mtazamo wake katika mambo mbalimbali, huu ndio mtazamo wangu katika mapenzi.


"Mwanamke anaekupenda kweli ni mama yako tu, kwa sababu ndio mwanamke pekee ata ukimkosea mara miilion lakini ukimuomba msamaha atakusamehe tu kwa sababu hana namna nyingine za kukusamehe.


Mwanamke yoyote akikupenda jambo la kwanza unatakiwa ujue amekupendea nini. Ukimpata mwanamke ukangundua anakupenda kutoka moyoni na wewe umempenda basi mpe moyo wako.


Ukimpenda Mwanamke kutoka moyoni lakini ukangundua anakupendea pesa basi mpe pesa(problem solved)! Kila mtu anaekupenda mpe kile anachokihitaji kutoka kwako Ili mradi kiwe ndani ya uwezo wako. Kwanini uidhulumu nafsi yako kwa kumuacha mwanamke unayempenda eti kisa anakupendea pesa na wakati kweli pesa unazo?

Give her Money bro, iridhishe nafsi yako life its too short but kuwa makini usifilisike kwa sababu ukifilisika utampoteza huyo mwanamke na wewe pia utapotea.

Mapenzi ni upendo na upendo ni matendo, cha muhimu hata huyo anayekupendea pesa akuonyeshe matendo ya upendo ilimradi akuridhishe nafsi yako kama wewe unavyomridhisha nafsi yake kwa kumpatia pesa yako.

Washukuru wanawake wote wanaokupenda kutoka moyoni au kwa pesa, kwa sababu kuna wanawake wengine hawawezi kukupenda hata ukiwa na pesa zako.


Note: Wanaume tutafute pesa siku hizi hakuna zali la mentali.
Huu ndio mtazamo wangu katika mahusiano ya mapenzi siku hizi. Huu ndio mtazamo wangu katika mahusiano ya mapenzi siku hizi. Reviewed by Love Psychologist on May 10, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.