Salaam;
Sitaki kuwachosha..! Mke wangu ni mjasiriamali anaondoka alfajiri anarudi jioni ukijumlisha na usumbufu wa magari na foleni mpaka kufika nyumbani anaingia saa 2 mpaka saa 3 kasoro. Hapo anafika anaoga tu na kulala. Maana anakuwa amechoka sana na majukumu ya mchana kutwa.
Ratiba yake ni ya jtatu-jpili.january-december. nilijaribu kumshauri apumzike jmosi na jpili ili apate muda wa kukaa na watoto na kufanya japo majukumu machache ya nyumbani. Lkn mke wangu hakukubali,siku za karibuni kijana wetu alianza mafundisho ya komunio,jumuiya wakamwambia lazma wazazi pia tusali jumuiya.
Akaanza kujisukuma kuwa anabaki jmosi nyumbani. Ingawa ameanza tena kugoma. Tatizo kubwa nguo zote hapa nyumbani,kuanzia anazovaa yy,nguo zangu zote,mashuka,kutandika kitanda kufanya usafi chumbani mpaka nguo zetu za ndani yaani boxer zangu na nguo zake ndani zote anafanya Dada wa kazi.
Yaani kifupi hapa nyumbani kazi zote zinafanywa na Dada wa kazi ikiwemo kutupikia nk. Kazi pekee ambayo hafanyi ni ile tu ya kutafuta watoto ndo mke wangu na mm tunafanya. Binafsi hii hali sipendezwi nayo,lkn mke wangu ukimwambia ni mkali sana..! Hebu naomba mnisaidie labda mm tu ndo nawaza vibaya labda si jambo baya linafanyika hivyo ktk familia zote.
Naomba kuwasilisha.
Ni Haki kwa Mke kuacha nguo zake za ndani afuliwe na Dada wa kazi?!
Reviewed by Love Psychologist
on
March 05, 2019
Rating:

No comments: