Sponsor

banner image

recent posts

Umama wa kambo umenishinda kabla hata haujaanza rasmi!



Kutoka Kwa Mdau


Ni kama mwaka niko katika mahusiano na huyu jamaa. Kiukweli tumeanza mahusiano akiwa na ndoa yake japo ilikuwa na misukosuko kadhaa na nadhani ndo sababu ya kumhurumia; naomba msinishambulie.

Penzi likashamiri nikataka kuolewa mke wa pili. Kwenda kwetu wazazi wakawa mbogo. Hawakuelewa japo dini inaruhusu. Mipango ya ndoa ilipodunda akampa mkewe talaka tena 3. Alipotaka twende tena kwa wazazi nimemwambia asubiri kwanza niwashawishi upya sababu walishachafukwa.

Kizaazaa kimekuja kwa watoto. Ana watoto wawili kutoka kwenye ndoa yake. Mmoja ana miaka 11 mwingine 7. Baada ya kuachana tukawa tunaishi pamoja kwenye nyumba niliyokuwa naishi awali yani yeye alihamia. Akawa anataka kumtoa mkewe kwenye nyumba ya familia tuhamie huko lakini nimeona si uungwana na alimuoa akiwa mdogo sana ndo alikuwa her everything atapata tabu.

December mwanzoni akaenda kuwachukua watoto wakaja kukaa nasi sababu hataki kwenda kuwaona kule. Sikuona tatizo sababu na mimi nina mtoto wa marehemu dada hapa namlea so anapata company.

Kwakweli huyu mtoto mkubwa hana adabu. Sijui kwenye kichwa chake mimi ananichukuliaje lakini sijapenda tabia yake.

Walipokuja baba yao akaleta TV kubwa zaidi. Huyu mtoto kila akizunguka sebuleni anamwambia mdogo wake "TV yetu, TV yetu". Haniamkii, anamwamkia baba yake tu, ananiita dada Zara hata baada ya baba yake kumwambia mimi ni mama na si kwamba mimi ni mdogo sana kwa mama yake, pamoja na vi-attitude kibao.

Sasa weekend iliyopita ndo kanichosha kabisa. Baba yao alisafiri Friday, wakati anaondoka wakamwambia daddy tumemiss kwenda beach akatoa cash 100,000 akanikabidhi ya kuwapeleka beach.

Sunday wakajiandaa tukaenda beach. Gharama za mafuta, chakula, icecream zikawa 56000 ikabaki 44000 kwenye pochi yangu. Kurudi nyumbani kaenda kachukua 22000. Sikugundua hadi kesho yake nimefika ofisini. Kurudi nyumbani nikawaita wote nikauliza nani kachukua pesa kwenye pochi yangu hakuna anayejibu. Mdogo akasema nilimuona kaka na hela nyingi. Kumuuliza akasema "nilichukua nusu tu."

Hivi kweli huyu mtoto anajiona na haki ya kugawana change na mimi kwa sababu aliitoa baba yake pesa? Amerudi jana nimemwambia cha kushangaza kaenda kumsimulia mama yake aliye mkoani then leo mama mkwe ananipigia simu ananiambia "Kama watoto unawashindwa mume utamuweza kweli? Hao ndo wafalme wa hiyo nyumba"

I was like wet the feck? Je, nimwambieje awarudishe kwa mama yao bila kuonekana nawachukia? Najiona nikishindwa kabisaaa!
Umama wa kambo umenishinda kabla hata haujaanza rasmi! Umama wa kambo umenishinda kabla hata haujaanza rasmi! Reviewed by Love Psychologist on March 05, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.