Leo nimeulizwa eti kati ya mke wangu na mama yangu mzazi nani nampenda zaidi? Sijajibu sababu mama mzazi na mke hawalinganishiki hata siku moja.
Uulizaji huo halafu nawe ukajibu eti mama au mke ujue unamdhihaki mama mzazi sababu mama anaplay party yake kama mama na mke anaplay party yake kama mke.
Ila ingeulizwa kati ya mke huyu na yule hapo nampenda zaidi nani ningejibu sababu wote ni wake zangu.
Vipi ninyi mwaonaje uulizwaji wa swali kama hili"mama na mke wampenda nani zaidi" yani limekaaje hili swali kwa upande wenu?
Nimechukia sana baada ya kuulizwa kati ya mama na mke nampenda nani
Reviewed by Love Psychologist
on
April 18, 2019
Rating:
No comments: