Sponsor

banner image

recent posts

Haya ndio yatakoyotokea mpenzi wako (KE) akienda chuo



Habari wadau,
Naona hili swala limekuwa gumu kuelezeka hasa kwa wale wanaotarajia aidha kuwasomesha wapenzi ama kuwasubiria wakasome kwa kuchaguliwa vyuoni halafu ndio waoe. Ukweli mchungu ni huu hapa jipimieni.

Chuo changamoto ni kwa asiyeweza kujitegemea kwa kila kitu na asiyejitambua.
Kama demu wako ana asili ya ushamba au wale wa kushikwa maskio yani mtu wa kuongozana na mashosti andika maumivu. Pia kama alikuwa anabanwa sana nyumbani ni tatizo jingine hilo.

Chuo ni sehemu nzuri ya kujifunza maisha ila mademu malimbukeni hufanya vituko vya kila aina hebu ona.

1. Kama alikuwa hajui club ataenda tu na pombe atakunywa...

2. Wewe au kwao hamna gari akibebwa kwenye gari na vijana wenye hayo mamlaka hachomoki...

3. Bata za kila weekend guaranteed kwa viwanja na mahoteli makubwa ya town, lazma sponsor akiomba utamu anapewa tu huku demu akidanganywa ataolewa na huyo jamaa baada ya chuo so hatokuwaza tena...

4. Akiwa kilaza jua kuna kipanga fisi wa darasani atapata fursa akimbana ghetto/hostel na kumpiga pindi kisha kulipwa penzi juu ya deka.

5. Kama alikuwa hajui kuvaa kuna mashosti atakutana nao huko watamvisha viwigi,makucha mpaka skin jeans na vikondom ili aonekane wa kisasa...

6. Kuna vijana wakishua watanashati 24/7 wenye mvuto na mamlaka kama wanaomiliki mageto makali,pesa,magari. Sio ajabu demu wako akakuona kolo tu huendani nae baada ya kuwa anatongozwa sana na watu highclass zaidi na kupelekwa viwanja vya maana.

7. Lecturers/wahadhiri wakware na walengaji lazma wamuombe mzigo kama atakuwa anamvuto wa kimapenzi ikiwa kajaza jaza ama ana rangi ya mtume ile. Hana ujanja coz akikataa the easy anaweza akawekewa vikwazo vya kitaaluma kama sup na carry hatimae akakubali the hard way.

8. Akiangalia we uwezo wako ghetto t.v chogo, full majaba outing mnaenda beach kimba kula madafu na azam chokstik na diamond karanga. Lazma aone unamchelewesha maisha tu.

ANGALIZO:
Mwaka wa kwanza unaeza maliza nae freshi ila hayo mara nyingi hutokea ndani ya mwaka wa pili wa chuo, we sikilizia tu! Nikushauri tu andaa backup plan in case haya yatatokea maana odds ni 90% likely kwa wasichana wengi!
Ukiona meseji hazijibiwi kwa wakati, namba inatumika sana kuanzia saa 4-6 usiku na pia hakujulii hali siku nzima mpaka umuanze na ukiulizia shida ni nini anakuwa mkali na visingizio ambavyo havikuwepo mwanzoni jua tayari.

Haya ndio yatakoyotokea mpenzi wako (KE) akienda chuo Haya ndio yatakoyotokea mpenzi wako (KE) akienda chuo Reviewed by Love Psychologist on May 03, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.