Sponsor

banner image

recent posts

Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa?



Habari zenu,sihitaji kashfa wala matusi hapa maana kuna watakatifu humu koo zao hazina singo mama wala walioachana..

 naomba kuuliza hivi singo mama siku hizi imekua ulemavu,kosa,dhambi au fursa!

Mimi sielewi maana naona Mara makongamano ya masingo maza,Mara sijui tamasha La singo mama,uwaunge mkono sijui uwachangie...jamani!!!

Hivi wanawake kwa nini tunapenda kujiona sisi ni waathirika wa kila jambo ambalo jamii inaliangali ktk mrengo tofauti...?

Mbona hakuna hayo mambo kwa wababa wanaolea watoto wenyewe?au wao hawakutani na changamoto za kimalezi?

Mimi binafsi sipendi na nachukia hii kitu (mniwie radhi kwa nitakaowakwaza)ila naona kama vile kujidhalilisha flani hivi...au ndo kutojiamini kama tunaweza!kwa staili hii tunataka usawa na wanaume...haitokaa itokee mpk Yesu arudi...!!!

Kama uliweza kubeba mimba,ikataliwe isikataliwe ukajifungua watoto au mtoto wako mwenyewe kwa nini usikomae mbona vijijini huko watu wanatelekezwa na wanalea watoto wao bila misaada?

Kama umetengana na mmeo au mmeachana kama unahisi huwezi kuwahudumia watoto si uwapeleke kwa baba yao?kama hutaki kaa nao Leo mwenyewe!!!

Yaani sasa hivi huku mijini masingo mama naona wanafanywa mitaji na watu wachache kujiingizia kipato na wenyewe wanaona kama wanapendwa kumbe hawajui ukiona umeitiwa fursa basi jua wewe ndo fursa yenyewe!!!

Wapo wanawake wengi wanalea watoto wao tena kwa shida na hawapigi kelele kimya kimya mpk wanakua!

Wamama wenzangu hii mitandao isifanye tujidhalilishe jamani...hebu tupambane kivingine sio mpk matangazo..maana huko kwenye mitandao siku hizi sijui wameonelea biashara ya Kuwakusanya singo mamaz inalipa kila mtu anaibuka na hoja zake!!

Tuinuke tupambane tusipende kujiweka nyuma!!!
Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa? Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa? Reviewed by Love Psychologist on May 04, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.