Sponsor

banner image

recent posts

Kijana mwenzangu ambaye bado haujaoa kama mimi



Sifa ni zake mwenyezi Mungu anayetujaalia afya njema mimi na wewe.
Vijana wenzangu ambao bado hatujaoa na tuna malengo ya kuoa naomba tuhakikishe kabisa kabla ya kuingia kwenye maisha ya ndoa tuwe tunajua na kutambua ni nini hasa maana ya maisha. Ndoa ni nini hasa, ni lipi lengo la kuingia kwenye ndoa,

Binafsi kwangu mimi maisha ni changamoto ambazo kiasili zilikuwapo, zipo na zitaendelea kuwepo, yaani naamini changamoto ni mazingira ambayo yametuzunguka sisi wanadamu katika kila siku za kuishi kwetu, naamini Mwenyezi Mungu aliniumba nije nipambane na mazingira (changamoto) mbalimbali nitakayokumbana nayo, hivyo sipaswi kuzikimbia bali lazima nipambane nazo ili kuzishinda, na hizi ni zile zenye kuniletea kikwazo katika kila hatua ya maisha yangu, kwani tunajifunza kwamba njia nzuri ya kutatua changamoto si kuikimbia bali ni kuikabili.

Ndugu zangu maisha ya ndoa si marahisi kama hatutaweza kuyajua maisha kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Si kila jambo laweza ufurahisha na kuutosheleza moyo na nafsi yako... Je walitambua hili..??? Si kila lenye kufanywa na kila umpendaye laweza kukuridhisha kila siku... Je walijua hili..??? Na unalichuliaje..???

Kijana mwenzangu ukielewa na kujifunza mengi juu ya mwanadamu, namna gani ya kuishi nae anapokuwa tofauti nawe, namna gani ya kuishi nae anapokuuzi, kukukasirisha, kukukera. Ukielewa namna gani ya kuishi na yule uliyemkera, kumuuzi na kumkasirisha.
Ukielewa kwamba binadamu tupo tofauti kimtazamo na kimuonekano, na kifikra.
Hakika kwa kiasi fulani utaweza ishi na mtu vizuri, na kiasi kikubwa utaweza angalau kubadilisha mtazamo wa mwenye kukosea na kumfanya mwenye kupatia mbele yako...

Mimi si mwandishi mzuri, ni mvivu kuandika ila ni muongeaji mzuri nina mengi, nimeandika machache, huenda yakatosha pia maana, sukari ni nzuri ila ikizidi kwenye chai hugeuka kuwa kero, hata chumvi ni nzuri kwenye chakula ila ikizidi huwa ni kero na chakula hakitolika. Lakini haiwezi kukufanya ushinde na njaa..

Ndoa si jambo dogo, ni jambo ambalo linahitaji utayari kifikra, kimawazo na kiakili... Usikurupuke
Kijana mwenzangu ambaye bado haujaoa kama mimi Kijana mwenzangu ambaye bado haujaoa kama mimi Reviewed by Love Psychologist on May 04, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.