Sponsor

banner image

recent posts

Sina amani wala furaha kwenye ndoa yangu, Nataka niondoke nimuachie kila kitu



Ni miaka kadhaa karibia mlongo mmoja kwenye ndoa, watoto wawili wa jinsia zote Mungu kajalia tumewapata.

Nyumba na Gari vyote tumejaaliwa katika ndoa yetu, Biashara inakuwa kwa kasi sana kiasi kizuri cha kuvutia.

Kiukweli sina amani na furaha katika ndoa yangu kabisa nataka niondoke home nikapange hata Chanika chumba kimoja nianze maisha yangu mwenyewe upya.

Sijafumania wala sijakosewa ila naona maisha yangu na mke wangu kwa sasa tunakuwa na mitazamo miwili tofauti, fikra zake na fikra zangu zimekuwa tofauti.

Kwa roho safi nataka nimkabidhi kadi za magari na hati ya nyumba kwa faida ya watoto kisha niondoke nikaanze maisha upya ila yawe maisha yangu mwenyewe pekee yangu. Nahisi ntakuwa na furaha zaidi nikiwa pekee yangu.

Ndugu zangu naomba ushauli kwenu kama mwana jamii na kama binadamu mwenzenu.


Asanteni sana.


Mrejesho wa kweli

Kiukweli nampenda mke sana, siwezi kumwacha aisee mtoto mzuri vile nimwache .! Itakuwa nimetenda Dhambi ya kumi na moja ( kujitesa bila sababu )
Sina amani wala furaha kwenye ndoa yangu, Nataka niondoke nimuachie kila kitu Sina amani wala furaha kwenye ndoa yangu, Nataka niondoke nimuachie kila kitu Reviewed by Love Psychologist on May 04, 2019 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.